Vitamin E Softgel
Viungo:
Vitamin E
.
Kazi Na Faida Zake
- Ni antioxidant yenye nguvu
- Kuzuia na kuondoa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu ya moyo, magonjwa ya ubongo na mishipa ya damu ya ubongo
- Huzuia saratani
- Yafaa kwa matatizo ya hedhi na ya uvimbe wa kwenye matiti
- Huulinda mfumo wa neva usivamiwe na radikali huru, kwa hiyo huboresha kumbukumbu na kuzuia kuzeeka haraka kwa mfumo wa neva
Yafaa Kutumiwa Na:
- Watu wanaoshindwa kupata kiwango cha kutosha cha siku cha vitamini E
- Watu waliodhamiria kuepuka magonjwa na moyo, ubongo na mishipa ya damu
- Watu wenye umri mkubwa
- Wanawake wenye matatizo ya kabla ya hedhi, matatizo ya uvimbe kwenye matiti, madoa meusi juu ya ngozi, matatizo ya hedhi, n.k.
Maelezo Muhimu:
Vitamini E ni neno linalojumuisha kundi la mchanganyiko wa vitu vinavyoyeyuka ndani ya mafuta vyenye tabia ya antioxidant. Mtu mzima mwenye afya anahitaji miligramu 15 za vitamini E kila siku kutoka kwenye chakula .
Vitamini E Na Kuzuia Madhara Ya Oksijeni:
Tabia ya vitamini E ya kuzuia madhara yatokanayo na oksijeni ni muhimu katika kudumisha ukamilifu na uthabiti wa utando wa nje wa seli. kwa mfano, vitamini E hulinda seli za mapafu ambazo kila wakati huguswa na oksijeni na chembechembe nyeupe za damu (white blood cells) zinazotusaidia kupambana na maradhi.
Vitamini E yaweza kuwa na msaada kwa watu wenye kisukari. Husaidia kazi ya insulin na kuboresha uvunjaji wa glucose kwa kupunguza shinikizo la oksijeni.
Kama antioxidant yenye nguvu, vitamini E husaidia kuzuia saratani, magonjwa ya moyo, kiharusi, mtoto wa jicho, na baadhi ya dalili za kuzeeka.
Kulinda Mfumo Wa Moyo Na Mishipa Ya Moyo:
Vitamini E hulinda kuta za ateri na kuzuia chlesterol mbaya- low-density lipoprotein (LDL) - zisiunguzwe na oksijeni . Kuunguzwa kwa LDL ndiyo mwanzo wa kuziba kwa ateri. Vitamini E pia huitinza damu iwe nyepesi kwa kuzuia chembechembe za damu (platelets) kugandana. Kuwa na kiwango kizuri cha vitamini E mwilini huepusha uwezekano wa kupata shinikizo la moyo au kiharusi.
Kupambana Na saratani:
Kama kizuia kansa, vitamini E huzilinda seli na DNA zisigeuka kuwa seli mbaya za kansa. Hupunguza uvimbe wakati huo huo ikiimarisha kinga za mwili na kuvizuia vitu vilivyotegemewa kugeuka kuwa seli za kansa.
Kwa Afya Ya Wanawake:
Wanawake wenye matatizo ya uvimbe kwenye maziwa (fibrocystic breast disease) hupata nafuu kwa kutumia vitamini E.Dalili za fibrocystic breast disease ni maumivu makali kwenye maziwa, wakati mwingine kukiwa na uvimbe, ukianza siku chache kabla ya kuanza hedhi. Madoa ya uzee au ya mionzi ya jua yanaweza kuondoka kwa kutumia vitamini E..
Kwa Mfumo Wa Neva
Bidhaa hii hulinda mfumo wa neva kwa kulinda ngozi ya nje (myelin sheaths) ya neva. Inaonekana pia kuzuia kuchoka kwa ubongo kunakotokana na umri, labda ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa alzheimer. Ugunduzi wa karibuni umeonyesha kuboreshwa kwa kumbukumbu za vitu vya karibuni kwa wazee waliotumia vitamini E. Pamoja na kwamba haikuongezei maisha, inaboresha maisha yako kadiri unavyokuwa mzee. br>
<<<<< MWANZO